Elizabeth Cady Stanton
Elizabeth Cady Stanton (12 Novemba 1815 - 26 Oktoba 1902) alikuwa mwanamke Mmarekani aliyejihusisha na harakati za kijamii, hasa ukomeshaji wa vitendo vilivyowanyima wanawake haki ya kupiga kura, na kiongozi shupavu katika harakati za haki za wanawake akishirikiana na Susan B.Anthony. Tamko lake la maoni, lililowasilishw katika mkutano wa kwanza wa haki za wanawake uliofanyika mwaka 1848 katika jiji la Seneca Falls, New York, husifiwa kuwa tamko la kwanza la kuwaunganisha wanawake katika kushiriki harakati za kutetea haki za wanawake, ikiwemo haki ya wanawake kupiga kura.[1].
Stanton alikuwa amepata elimu nzuri. Katika kipindi hiko suala la elimu kwa wanawake lilikuwa halipewi kipaumbele. Aliolewa na Henry Stanton, ambaye alipigania kutokemeza utumwa. Walikuwa na watoto saba. Alikuja kuvutiwa na utetezi wa haki za wanawake alipohudhuria mkutano wa kutokemeza utumwa duniani uliofanyika London. Yeye na Lucretia Mott, mwanaharakati mwingine, walichukizwa kwa sababu wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuwa sehemu ya watu wanaohudhuria kikao. Kwa sababu hiyo, walianzisha mkutano wao wa haki za wanawake.
Mkutano wa kwanza ulikuwa mwaka 1848 katika mji wa Seneca Falls, New York. Stanton aliandika tamko la maoni lililohusu kuhitaji mabadiliko. Baadhi ya mabadiliko waliyohitaji ni kuruhusu wanawake kupiga kura na kuwafanya wawe na haki sawa na wanaume katika jamii. Tamko hilo lilisainiwa na wanawake katika mkutano.
Stanton aliendelea kupigania haki za wanawake kwa kusambaza makubaliano yaliyosainiwa katika mkutano katika jiji lote la New York. Makubaliano yaliyosainiwa na wanawake yalidhamiriwa kusukuma bunge la New York katika kupitisha kifungu cha wanawake walioolewa kuwa na haki ya umiliki New York.
Mwaka 1851, Stanton alikutana na Susan B. Anthony, mwanaharakati mwingine maarufu. Stanton na Anthony walifanya kazi pamoja kwa kipindi kirefu. Kwa pamoja waliandika hotuba, makala na vitabu. Stanton na Anthony walikuwa viongozi wa harakati za haki za wanawake kwa zaidi ya miaka hamsini. Stanton na Matilda Gage waliandika Tamko au Haki ambayo iliwasilishwa na Susan B.Anthony mwaka 1876 katika Philadephia Centennial.
Stanton alisafiri maeneo mbalimbali nchini humo na alikuwa kama rais wa haki za wanawake kupiga kura kitaifa. Katika kusafiri kwake aliongelewa kuhusu mambo ya kijamii ya sasa yanayohusiana na haki za wanawake. Kati ya hayo mambo ilikiwemo sheria ya talaka na kulea watoto.
Katika miaka yake ya baadae, Stanton alikuwa bado mwanasiasa hai, hata kama akusafiri sana. Aliandika, pamoja na Anthony na Gage, vitabu vilivyoitwa historia ya haki ya wanawake ya kupiga kura kuanzia 1881 mpaka 1885. Pia alichapisha Biblia ya wanawake. Aliandika kitabu kuhusu maisha yake kilichoitwa "Miaka themanini na zaidi" (Eighty years and more).
Stanton alifariki mwaka 1902 katika jiji la New York, miaka kumi na nane kabla wanawake hawajaruhusiwa kupiga kura.
Marejeo
- ↑ "Elizabeth Cady Stanton Dies at Her Home.". New York Times. October 27, 1902. Retrieved 2007-10-31. "Mrs. Elizabeth Cady Stanton died at 3 o'clock yesterday afternoon at her home in the Stuart Apartment House, 250 West Ninety-fourth Street. Had she lived until the 12th of next month she would have been 87."
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elizabeth Cady Stanton kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |