Jimbo Katoliki la Rumbek
Jimbo la Rumbek (kwa Kilatini Dioecesis Rumbekensis) ni mojawapo kati ya majimbo 7 ya Kanisa Katoliki nchini Sudan Kusini na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Yote yanaunda kanda ya Kanisa yenye makao makuu katika Jimbo Kuu la Juba.
Askofu wake wa mwisho alifariki mwaka 2011 na tangu hapo hakukuwa na mwingine hadi Machi 2021 alipoteuliwa Christian Carlassare, M.C.C.I.
Takwimu
Eneo la jimbo lina kilometa mraba 60,000, ambapo kati ya wakazi 1,561,000 (2017) Wakatoliki ni 182,000 (sawa na 11.7%). Parokia ziko 13, mapadri ni 29 na watawa 64.
Viungo vya nje
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Rumbek kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |