Jimbo Katoliki la Yei
Jimbo la Yei (kwa Kilatini Dioecesis Yeiensis) ni mojawapo kati ya majimbo 7 ya Kanisa Katoliki nchini Sudan Kusini na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Yote yanaunda kanda ya Kanisa yenye makao makuu katika Jimbo Kuu la Juba.
Askofu wake ni Erkolano Lodu Tombe (tangu mwaka 1985).
Takwimu
Eneo la jimbo lina kilometa mraba 46,000, ambapo kati ya wakazi 740,250 (2012) Wakatoliki ni 348,620 (sawa na 47.1%). Parokia ziko 7, mapadri ni 18 na watawa 11.