Jumatano ya Majivu

A priest marks a cross of ashes on a worshipper's forehead.
Mkristo akipakwa majivu siku hiyo.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Jumatano ya Majivu, katika kalenda ya mwaka wa Kanisa la Magharibi[1], ni siku ya kwanza ya kwaresima, walau kwa madhehebu mengi[2][3][4][5][6][7][8][9][10][11][12][13][14][15] (katika liturujia ya Milano Kwaresima inaanza Jumapili inayofuata, hivyo majivu yanapakwa siku hiyo, si Jumatano[16][17]).

Jina

Jina linatokana na desturi katika Kanisa Katoliki ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka[18][19].

Yesu Akishawishwa Jangwani, James Tissot, Brooklyn Museum.

Mfungo

Kwa kawaida siku hiyo unaanza mfungo wa siku 40 kabla ya sherehe ya Pasaka. Kipindi hicho kinatunza kumbukumbu ya Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

Tarehe

Tarehe ya Jumatano ya Majivu hutegemea ile ya Pasaka. Ni siku ya kufunga ya 40 kabla ya Pasaka; ilhali katika desturi hii siku za Jumapili hakuna kufunga, ni siku ya 46 kabla ya sikukuu, maana kuna Jumapili 6 ndani ya Kwaresima.

Tarehe ya mapema inayowezekana ni 4 Februari, tarehe ya mwisho inayoweza kutokea ni 10 Machi.

Filamu

  • Ash Wednesday (1958 film)
  • Ash Wednesday (1973 film)
  • Ash Wednesday (2002 film)

Tanbihi

  1. Melton, J. Gordon (2011). "Ash Wednesday", Religious Celebrations: An Encyclopedia of Holidays, Festivals, Solemn Observances, and Spiritual Commemorations 1. Santa Barbara: ABC-CLIO, 49–50. ISBN 978-1-59884-206-7. 
  2. Scanlon, Leslie (7 February 2005). Ash Wednesday: What do Presbyterians do? (en-US).
  3. (2009) Feasting on the Word: Year C, Volume 2: Lent through Eastertide. Presbyterian Publishing Corporation, 22. ISBN 9781611641189. 
  4. Koonse, Emma (5 March 2014). Ash Wednesday Today, Christians Observe First Day of Lent. The Christian Post. “Although some denominations do not practice the application of ashes to the forehead as a mark of public commitment on Ash Wednesday, those that do include Catholics, Anglicans, Lutherans, Methodists, Presbyterians, and some Baptist followers.”
  5. Sleeth, Nancy (23 February 2017). How do you observe Lent? (en-US).
  6. Lent: Preparation for Easter | HOLINESS TODAY. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-03-11. Iliwekwa mnamo 2024-02-10.
  7. First Day of Lent, Ash Wednesday (en-CA). Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-02-14. Iliwekwa mnamo 2024-02-10.
  8. Ahlgrim, Ryan. "Remember that you are dust", Mennonite World Review, 13 February 2018. (en-US) 
  9. Harader, Joanna. "Preparing to enter LentKigezo:Sndthoughts on Ash Wednesday", Mennonite World Review, 18 February 2015. (en-US) 
  10. Moravian Women's Association (March 2017). Lent around the world. The Moravian Church British Province. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-02-14. Iliwekwa mnamo 2024-02-10.
  11. Ash Wednesday 2018 Worship Resources (en-US).
  12. Moderator's Lent Message 2020 (English). United Church of Canada (17 February 2020). Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-02-21. Iliwekwa mnamo 2024-02-10.
  13. Wagner, Abp. Wynn (6 February 2011). A Catechism of the Liberal Catholic Church, 4th, BookBaby, 53. ISBN 9781609849306. [dead link]
  14. Cabie, Honor Blanco. "Ash Wednesday ushers in time of remorse", Manila Standard, 14 February 2018. (en) 
  15. Ash Wednesday Ideas (en). Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-10-21. Iliwekwa mnamo 2024-02-10.
  16. Il Sussidiario, Giorno delle Ceneri: Cos'è il rito delle Ceneri Archived 14 Julai 2014 at the Wayback Machine
  17. Sapere, Perché il Carnevale ambrosiano si festeggia in ritardo rispetto al resto d’Italia? Archived 24 Mei 2014 at the Wayback Machine
  18. (14 September 2011) The Roman Missal [Third Typical Edition, Chapel Edition], 210. ISBN 9781568549903. 
  19. (29 November 2019) Protestant Worship: A Multisensory Introduction for Students and Practitioners (in en). Abingdon Press, 182. ISBN 978-1-5018-4266-5. 

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jumatano ya Majivu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.