Kinyonga (kundinyota)

Nyota za kundinyota Kinyonga (Chamaeleon) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Kinyonga - Chamaeleon

Kinyonga (kwa Kilatini na Kiingereza Chamaeleon) [1] ni jina la kundinyota ndogo kwenye angakusi.

Mahali pake

Kinyonga lipo karibu na ncha ya anga ya kusini. Linapakana na kundinyota Nzi ( Musca), Mkuku (en:Carina) na Panzimaji (en:Volans) upande wa kaskazini, Meza (en:Mensa) upande wa mashariki, Thumni (Octans) upande wa kusini na Ndege wa Peponi (Apus) upande wa magharibi.

Jina

Kinyonga linapatikana kati ya makundinyota yaliyobuniwa tangu mabaharia Wazungu walipozunguka Dunia yote katika karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota za kusini. Hazikutajwa katika vitabu vya Wagiriki wa Kale au vya Waarabu. Kundinyota hili ilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi Pieter Dirkszoon Keyser na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika globu ya nyota ya Petrus Plancius. Baadaye ilipokelewa katika "Uranometria" ya Johann Bayer[2].

Keyser alitumia jina la Kiholanzi la Het Chameljoen (Kinyonga) iliyotajwa baadaye kwa jina la Kigirikiki „Chamaeleon“.

Leo iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [3]. Kifupi rasmi ni ‘Cha’.

Nyota

Nyota angavu zaidi ni α Alfa Chamaeleontis yenye mwangaza unaoonekana wa 4.07 mag ikiwa umbali wa Dunia wa miakanuru 63.5[4]

Kwa jumla kuna nyota nne angavu kiasi, nje ya αCha ni βCha (mag 2.2), γCha (mag 4.1) na δCha (mag 5.5).

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Chamaeleon" katika lugha ya Kilatini ni "Chamaeleontis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Chamaeleontis, nk.
  2. Allen (tazama marejeo) hakuwa na habari za Placius hivyo aliandika ni Bayer aliyetangaza Kinyonga mara ya kwanza.
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  4. Alpha Cha (Alpha Chamaeleontis), tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje