Panzimaji (kundinyota)

Nyota za kundinyota Panzimaji (Volans) katika sehemu yao ya angani

Panzimaji (kwa Kilatini na Kiingereza Volans) [1]. ni jina la kundinyota kwenye angakusi ya Dunia yetu. Lipo jirani na kundinyota la Mkuku (Carina.

Jina

Panzimaji inapatikana kati ya makundinyota yaliyobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka dunia yote yaani karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota za kusini. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi Pieter Dirkszoon Keyser na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika globu ya nyota ya Petrus Plancius. Keyser alitumia jina la Vliegendenvis (samaki anayeruka yaani panzimaji)[2] iliyotafsiriwa na Bayer kwa kilatini kuwa « Piscis Volans » iliyoendelea kufupishwa baadaye kuwa « Volans ».

Nyota

Kundinyota la Panzimaji lina nyota chache na dhaifu kiasi. Angavu zaidi ni β Beta Volantis yenye uangavu wa 3.77 mag ikiwa umbali wa Dunia wa miakanuru 108.

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Volans" katika lugha ya Kilatini ni "Volantis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Volantis, nk.
  2. "Star Tales Volans". Ian Ridpath. Iliwekwa mnamo 14 Agosti 2015.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)