Kisonono
Kisonono au kisalisali ni maradhi ya zinaa ambayo husababishwa na bakteria zinazofahamika kisayansi kama Neisseria gonorrhoeae. Bakteria hizo hushambulia utandotelezi unaozunguka sehemu za siri.
Ingawa kwa makisio maambukizi 360,000 ya kisonono huripotiwa kila mwaka nchini Marekani, wataalamu wamekisia kuwa watu karibia 650,000 huambukizwa kwa mwaka. Kimataifa yanakadiriwa kuwa kati ya milioni 33 na 106 kwa mwaka. Wagonjwa ni 0.8% ya wanawake wote na 0.6% ya wanaume wote.
Kama ilivyo klamidia, kisonono nayo huwa haionyeshi dalili. Kisonono ikiwepo huwa na dalili kama zile za klamidia ambazo huhusisha mauvimu wakati wa kukojoa na kutokwa kwa maji yanayonuka au usaha katika uke au uume.
Kisonono huonekana kwa urahisi kwa wanaume ambao hutoa usaha kutoka katika mfereji wa mkojo (urethra). Huanza kidogo, lakini huongezeka na huwa mwingi na kusababisha kusikia haja ya kukojoa mara kwa mara huku kukiwa na maumivu.
Kisonono ikisambaa na kufikia tezi kibofu, mfereji wa mkojo huziba kwa kiasi fulani. Kwa wanawake maambuki hutokea katika urethra, uke au mlango wa uzazi (cervix). Ingawa mwasho unaotokana na majimaji katika uke unaweza kuwa mkubwa, mara nyingi dalili hizi huwa ni chache au hamna kabisa katika hatua za awali.
Kisonono isiyotibiwa inaweza kusababisha PID (Pelvic Infiammatory disease) kwa wanawake. Watoto wanaozaliwa na mama wenye kisonono huwa na hatari ya kuambukizwa wakati wa kuzaliwa; maambukizo haya yanaweza kusababisha magonjwa ya meno kwa wachanga.
Uchunguzi wa ugonjwa hufanywa kwa kuchungunza usaha kutoka katika uke au uume au mkojo kwa uwepo wa Neisseria gonorrhoeae.
Kisonono iliongezeka kwa kiasi kikubwa Marekani mnamo miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980, hadi kukaribia kufikia kiwango cha magonjwa ya mlipuko (epidemic proportions) kwa vijana wanaobalehe na watu wa umri wa kati.
Kisonono hutibiwa kwa antibiotiki kadhaa, ingawa maambukizi yamekuwa na ukinzani juu ya tiba ya baadhi ya madawa katika miongo ya nyuma. Moja kati ya mambo magumu katika kupambana na kisonono ni kutafuta mahusiano yote ya kimapenzi ya nyuma ya aliyeambukizwa ili kuweza kuzuia usambaaji zaidi wa ugonjwa.
Tanbihi
- ↑ "Prophylaxis for Gonococcal and Chlamydial Ophthalmia Neonatorum in the Canadian Guide to Clinical Preventative Health Care". Public Health Agency of Canada. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-10. Iliwekwa mnamo 2016-10-16. Unknown parameter
|=
ignored (help)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kisonono kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |