Kipanyanyasi-milia
Kipanyanyasi-milia | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kipanyanyasi-milia wa kawaida katika Msitu wa Kakamega (Lemniscomys striatus)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 11:
|
Vipanyanyasi-milia ni wanyama wagugunaji wa jenasi Lemniscomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea katika mbuga za Afrika.
Maelezo
Panya hawa wana mlia mweusi mgongoni na spishi wengine zina milia na madoa mengine pia. Urefu wa mwili ni mm 90-140, urefu wa mkia ni mm 95-150 na uzito ni g 18-70.
Kwa ujumla huzingatiwa kukiakia wakati wa mchana, lakini angalau spishi kadhaa zinaweza kukiakia usiku. Hula majani, mizizi na mbegu na mara kwa mara wadudu pia.
Kuna wachanga hadi 12 kwa kila mkumbo, lakini 4-5 ni kawaida zaidi. Wanaweza kuwa na mikumbo minne katika kipindi cha chini ya miezi minne. Wastani wa matarajio ya muda wa kuishi ni mfupi sana, porini mara nyingi mwaka mmoja tu, lakini L. striatus aliishi kwa karibu miaka 5 kifungoni.
Spishi
- Lemniscomys barbarus (Barbary striped grass mouse)
- Lemniscomys bellieri (Bellier's striped grass mouse)
- Lemniscomys griselda (Griselda's striped grass mouse)
- Lemniscomys hoogstraali (Hoogstraal's striped grass mouse)
- Lemniscomys linulus (Senegal one-striped grass mouse)
- Lemniscomys macculus, Kipanyanyasi Milia-hudhurungi (Buffoon striped grass mouse) – Kenya, Uganda
- Lemniscomys mittendorfi (Mittendorf's striped grass mouse)
- Lemniscomys rosalia, Kipanyanyasi Mlia-mmoja (Single-striped grass mouse) – Kenya, Tanzania
- Lemniscomys roseveari (Rosevear's striped grass mouse)
- Lemniscomys striatus, Kipanyanyasi-milia wa Kawaida (Typical striped grass mouse) – Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda
- Lemniscomys zebra, Kipanyanyasi-milia wa Heuglin (Heuglin's striped grass mouse) – Kenya, Tanzania, Uganda
Picha
-
Barbary striped grass mouse
-
Kipanyanyasi mlia-mmoja