Malaika mkuu

Mchoro wa Guido Reni ukionyesha ushindi wa malaika mkuu Mikaeli dhidi ya Shetani, 1636.

Malaika mkuu (kwa Kigiriki ἀρχάγγελος arkh+angelos)[1] ni jina la heshima kwa baadhi ya malaika wenye hadhi ya juu kati ya viumbe vya kiroho.

Msingi wa imani hiyo ni kwamba kila malaika ameumbwa peke yake na tofauti na wengine wote, na kwamba katika kumtumikia Mungu aliyewaumba wanashirikiana kwa ngazi.

Katika Ukristo

Biblia ya Kikristo inatumia jina hilo mara mbili: katika Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike 4:16 na katika Waraka wa Yuda 1:9, ambapo linamhusu malaika Mikaeli.

Kanisa Katoliki na baadhi ya madhehebu mengine ya Kikristo wanaheshimu malaika wakuu watatu tu: Mikaeli, Gabrieli na Rafaeli[2].

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.