Matengenezo ya Meiji
Matengenezo ya Meiji (kwa Kijapani 明治維新 meiji ishin, kwa Kiingereza Meiji restauration) kilikuwa kipindi cha mabadiliko makubwa nchini Japani kuanzia mnamo mwaka 1866 yaliyotokea hasa chini ya utawala wa Kaisari Meiji (1867 - 1912).
Mabadiliko hayo yalihusika siasa, utamaduni na uchumi wa Japani. Yalisababisha nchi hiyo kuvuka katika kipindi kifupi kutoka jamii ya kijadi kwenda uchumi wa viwandani.
Utangulizi
Mnamo karne ya 19 Japani ilikuwa nchi iliyofungwa kwa wageni wa nje tangu karne mbili. Wafanyabiashara kutoka Uholanzi peke yao waliruhusiwa kufika kwenye kisiwa kidogo cha Dejima karibu na mji wa Nagasaki pekee.
Kisiasa serikali kuu ilikuwa mikononi mwa shogun, kabaila mkubwa aliyetawala kwa jina la tenno au kaisari ya Japani. Tangu karne ya 17 cheo cha tenno kilikuwa jina tu, matenno walifungwa ndani ya ikulu yao na maamuzi yote yalichukuliwa na shogun. Cheo hiki kilirithiwa katika nasaba ya Togukawa tangu mwaka 1603.
Utawala wa shogun haukuwa moja kwa moja bali ulikuwa ngazi ya juu katika mfumo wa ukabaila. Daimyo au makabaila wakubwa walisimamia majimbo yao walipopokea kodi za wenyeji. Cheo cha daimyo pamoja na utawala juu ya jimbo lake kilirithiwa ndani ya familia fulani. Chini yao kulikuwa na makabaila wadogo ambao wengi wao walikuwa samurai wa tabaka la askari.
Mwaka 1853 kikosi cha manowari za Marekani chini ya nahodha Perry kiliingia kwenye bandari ya Kanagawa na Perry alidai kukutana na wawakilishi wa serikali akiwa na maagizo ya kulazimisha serikali ya Japani kukubali mkataba wa biashara na Marekani. Alikataa kuondoka akatishia kutumia silaha zake na hivyo serikali ya Shogun ilikubali. Mikataba kadhaa ilizipa nchi za kigeni haki ya kufungulia balozi na vituo vya biashara ndani ya Japani.
Hatua hiyo ilimaanisha kuachana na utaratibu wa karne mbili na sasa wageni walianza kuonekana katika miji ya Japani. Hii ilisababisha upinzani dhidi ya Shogun kwa upande wa sehemu ya makabaila. Daimyo kadhaa walishambulia meli za kigeni zilozokaribia pwani zao na kushambulia wageni. Hapo manowari za nchi za Ulaya zililipiza kisasi na majeshi ya daimyo kadhaa.
Baada ya shogun (mtawala wa nchi) kukubali kuingia kwa wageni katika Japan alidhoofishwa machoni pa daimyo (makabaila wakubwa) na upinzani uliongezeka.
Upinzani wa daimyo dhidi ya shogun
Daimyo wengine walitambua ya kwamba jamii na jeshi la Japani lilikosa uwezo wa kushindana na hao watu wa nje waliokuwa na manowari na silaha zenye uwezo uliopita yote yaliyojulikana katika Japani. Walitambua pia ya kwamba msingi wa uwezo huo ulikuwa katika elimu na sayansi ya wageni.
Wengine waliona sababu ya udhaifu katika athira ya China katika utamaduni wa Japani na utawala wa Shogun kuwa dalili yake ya kisiasa. Fundisho lilisambaa lililodai kurudi pale palipoaminiwa ni mizizi ya Kijapani ya kweli pamoja na kuinua nafasi ya tenno au kaisari katika dola.
Kaisari Komei (1831 - 1867) alikuwa tenno katika kipindi cha vurugu kutokana na kufika kwa Wamarekani na wengineo. Mwaka 1858 shogun alituma balozi kwake na mara ya kwanza baada ya karne 2 tenno alihusishwa tena na siasa. Komei aliunga mkono daimyo na samurai waliopigana na wageni.
Kupinduliwa kwa mfumo wa shogun na kurudishwa kwa tenno madarakani
Mwaka 1866 Tokugawa Yoshinobu alikuwa shogun baada ya kifo cha mtangulizi. Alijitahidi kufanya marekebisho katika jeshi na serikali na kutafuta upatanisho na wafuasi wa tenno. Lakini Tenno Komei alikufa baada ya muda mfupi na mwanawe Mutsuhito (Meiji) alipokea cheo mnamo Februari 1867 akiwa na umri wa miaka 14 tu. Tenno kijana alikuwa zaidi chini ya athira ya upinzani.
Kundi la daimyo liliendelea kushikamana dhidi ya shogun walielekea mfumo wa serikali ambako taifa lingetawaliwa na kamati ya madaimyo badala ya shogun. Tarehe 9 Novemba 1867 Shogun Tokugawa Yoshinobu alimwandikia tenno barua alipojitolea kuachana na madaraka yake na kuyarudisha kwa kaisari kwa sababu huko nyuma shogun wa kwanza aliwahi kupokea madaraka kutoka kwa tenno.
Tarehe 3 Januari 1868 tenno mpya -aliyeshauriwa na kuongozwa na madaimyo wa upinzani- alitoa tamko rasmi la kwamba alipokea ombi la shogun na alichukua tena madaraka yote katika dola. Tarehe hiyo inatazamwa kama siku ya kurudishwa kwa tenno yaani Kaisari wa Japani katika nafasi ya utawala. Tenno alichukua jina la "Meiji" ambalo limekuwa jina la kipindi hiki chote.
Mapinduzi kutoka juu
Hali halisi tenno hakutawala mwenyewe: aliendelea kufuata ushauri na maagizo wa kundi la madaimyo na samurai walioshikamana kulenga mabadiliko makubwa yaliyotakiwa kuongeza uwezo na nguvu ya Japani.
Marejeo
- Akamatsu, Paul (1972). Meiji 1868: Revolution and Counter-Revolution in Japan. New York: Harper & Row. uk. 1247.
- Beasley, William G., . (1972). The Meiji Restoration. Stanford: Stanford University Press.
{cite book}
:|first=
has numeric name (help) - Beasley, William G. (1995). The Rise of Modern Japan: Political, Economic and Social Change Since 1850. New York: St. Martin's Press.
- Craig, Albert M. (1961). Chōshū in the Meiji Restoration. Cambridge: Harvard University Press.
- Jansen, Marius B. (1986). Japan in Transition: From Tokugawa to Meiji. Princeton: Princeton University Press.
{cite book}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - Jansen, Marius B. (2000). The Making of Modern Japan. Cambridge: Harvard University Press.
- Murphey, Rhoads (1997). East Asia: A New History. New York: Addison Wesley Longman.
- Satow, Ernest Mason. A Diplomat in Japan. ISBN 4-925080-28-8.
- Wall, Rachel F. (1971). Japan's Century: An Interpretation of Japanese History since the Eighteen-fifties. London: The Historical Association.
- Breen, John, 'The Imperial Oath of April 1868: ritual, power and politics in Restoration Japan', Monumenta Nipponica,51,4 (1996)
- Francisco Barberan & Rafael Domingo Osle, Codigo civil japones. Estudio preliminar, traduccion y notas (2 ed. Thomsons Aranzadi, 2006).
- Harry D. Harootunian, Toward Restoration (Berkeley: University of California Press, 1970), "Introduction", pp 1 – 46; on Yoshida: chapter IV "The Culture of Action – Yoshida Shōin", pp 184 – 219.
- Najita Tetsuo, The Intellectual Foundations of Modern Japanese Politics (Chicago & London: University of Chicago Press), chapter 3: "Restorationism in Late Tokugawa", pp 43 – 68.
- H. Van Straelen, Yoshida Shōin, Forerunner of the Meiji Restoration: A Biographical Study (Leiden: E. J. Brill, 1952).
- David M. Earl, Emperor and Nation in Japan (Seattle: University of Washington Press, 1972), on Yoshida: "Attitude toward the Emperor/Nation", pp 161 – 192. Also pp. 82 – 105.
- Marius B Jansen, Sakamoto Ryōma and the Meiji Restoration (New York: Columbia University Press, 1994) especially chapter VIII: "Restoration", pp 312 – 346.
- W. G. Beasley, The Meiji Restoration (Stanford, California: Stanford University Press, 1972), especially chapter VI: "Dissenting Samurai", pp 140 – 171.
- Conrad Totman, "From Reformism to Transformism, bakufu Policy 1853–1868", in: T. Najita & V. J. Koshmann, Conflict in Modern Japanese History (New Jersay: Princeton University Press, 1988), pp. 62 – 80.
- Jansen, Marius B.: The Meiji Restoration, in: Jansen, Marius B. (ed.): The Cambridge history of Japan, Volume 5: The nineteenth century (New York: Cambridge UP, 1989), pp. 308–366.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Matengenezo ya Meiji kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |