Mkomamanga

Mkomamanga
(Punica granatum)
Mkomamanga mwenye matunda
Mkomamanga mwenye matunda
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Myrtales (Mimea kama mkarafuu)
Familia: Lythraceae (Mimea iliyo na mnasaba na mhina)
Jenasi: Punica
Spishi: P. granatum
L.

Mkomamanga au mkudhumani (Punica granatum) ni mti mdogo wa familia Lythraceae katika oda Myrtales. Matunda yake huitwa makomamanga au makudhumani. Asili yake ni eneo la Uajemi ya kisasa, lakini siku hizi hukuzwa katika Mashariki ya Kati, Kaukasi, Ulaya ya Kusini, Afrika ya Kaskazini ni chini ya Sahara, Asia ya Kati, ya Kusini na ya Kusini-Mashariki, Arizona na Kalifornia.

Picha