Mlima Sinai

Mahali pa mlima Sinai kwenye rasi ya Sinai
Mazingira ya mlima Sinai

Mlima Sinai (kwa Kiarabu: جبل موسى jabal Musa = mlima wa Musa) ni mlima wenye kimo cha mita 2,283 juu ya UB katika eneo la kusini la Rasi ya Sinai nchini Misri. Unajulikana pia kwa jina la Mlima Horeb au kwa jina lake la Kiarabu kama Gebel Musa (matamshi ya Kimisri) au Jabal Musa (matamshi ya Kiarabu sanifu).

Mlima Sinai unaaminiwa tangu kale kuwa ndio mahali ambako Musa alipokea amri kumi kutoka kwa Mungu wakati wa Wanaisraeli kuacha utumwa wa Misri.

Kilele cha mlima kina kanisa la Waorthodoksi lenye asili ya jengo la Kaisari Justiniano I la mwaka 532 na pia msikiti wa karne ya 12.

Monasteri ya Mt. Katarina iko kwenye mwanzo wa mlima.

Viungo vya Nje