Namba atomia
Namba atomia inataja idadi ya protoni katika kiini cha atomi. Idadi ya protoni kwakawaida huwa sawa na idadi ya elektroni za mzingo elektroni hivyo namba atomia inataja pia idadi ya elektroni.[1]
Atomi zenye namba atomia ileile ni za elementi moja zikionyesha tabia zilezile za kikemia isipokuwa mara chache isotopi zinaweza kuwa na tofauti ndogo. Atomi zenye namba atomia ileile lakini zinazotofautiana katika masi kwa sababu ya tofauti katika idadi ya neutroni huitwa isotopi ya elementi moja.
Katika mfumo radidia elementi hupangwa kufuatana na namba atomia. Idadi ya protoni katika kiini haibadiliki.
Marejeo
- ↑ Lakini katika hali ya ioni atomi inaweza kupokea elektroni ya ziada kutoka nje au kuachana na elektroni.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Namba atomia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |