Ng'ombe (zamani pia bakari) ni wanyama wakubwa wanaokula nyasi. Ni wanyama wanaofugwa kwa wingi sana kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi au pia kwa kuvuta plau au gari la kukokotwa.
Kwa asili kuna aina mbili za ng'ombe-kaya: ng'ombe wa Ulaya na ng'ombe wa Uhindi ambazo ni nususpishi za B. primigenius (B. p. taurus na B. p. indicus mtawalia, ingawa mara nyingi nususpishi hizo zinaainishwa kama spishi za B. taurus na B. indicus). Zinatoka kwa nususpishi za zamani B. p. primigenius na B. p. namadicus.
Siku hizi ni vigumu kufahamu nususpishi za ng'ombe, kwa sababu takriban aina zote za ng'ombe ni chotara sasa.
Ng'ombe hula nyasi na hutembea kwa kwato. Ng'ombe waliofugwa na binadamu walitokana na ng'ombe-mwitu ili kujipatia nyama na maziwa. Katika nchi nyingi hutumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika Mashariki ya Kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga na kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.
Wanacheua chakula chao na huwa na tumbo lenye vyumba vinne. Baada ya kula nyasi mara ya kwanza wanairudisha kutoka chumba cha kwanza cha tumbo na kuitafuna tena. Kwa njia hii wanapata lishe nyingi kutoka nyasi.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ng'ombe kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Indian Spotted Chevrotain (M. indica) · Yellow-striped Chevrotain (M. kathygre) · Sri Lankan Spotted Chevrotain (M. meminna)
Tragulus
Java Mouse-deer (T. javanicus) · Lesser Mouse-deer (T. kanchil) · Greater Mouse-deer (T. napu) · Philippine Mouse-deer (T. nigricans) · Vietnam Mouse-deer (T. versicolor) · Williamson's Mouse-deer (T. williamsoni)
Kuro (K. ellipsiprymnus) ·Mraye (K. kob) · Lechwe kusi (K. leche) · Lechwe wa Nili (K. megaceros) · Lechwe wa Upemba (K. anselli) ·Sheshe (K. vardonii)
Swala wa Cuvier (G. cuvieri) · Swala-jangwa (G. dorcas) · Swala mhindi (G. bennettii) · Swala-milima (G. gazella) · · Swala mwajemi (G. subgutturosa)Swala wa Neumann (G. erlangeri) · Swala wa Sahara (G. leptoceros) · Swala wa Saudia (G. saudiya) · Swala wa Speke (G. spekei)
Palawan Bearded Pig (S. ahoenobarbus) · Bearded Pig (S. barbatus) · Indo-chinese Warty Pig (S. bucculentus) · Visayan Warty Pig (S. cebifrons) · Celebes Warty Pig (S. celebensis) · Flores Warty Pig (S. heureni) · Oliver's Warty Pig (S. oliveri) · Philippine Warty Pig (S. philippensis) · Nguruwe-mwitu wa Ulaya (S. scrofa) · Timor Warty Pig (S. timoriensis) · Javan Pig (S. verrucosus)