Paradiso
Paradiso (kwa Kigiriki παράδεισος paradeisos kutoka Kiajemi cha zamani: پردیس, *paridayda- "eneo lililozungukwa na uzio" au bustani) ni jina la mahali pa amani kamili palipo tarajio kuu la waumini wa dini mbalimbali. Dini za Abrahamu zinatumia jina hilo la Edeni / Paradiso, linaloonyeshwa katika Kitabu cha Mwanzo cha Biblia kama mahali pa uumbaji wa binadamu, na hivyo kuchukuliwa kama kielelezo cha ulimwengu wa kabla ya dhambi ya asili, na vilevile kwa ule unaotarajiwa kuwepo milele.
Neno "paradiso" limeenea katika lugha nyingi (paradis, paradisus, paradise n.k.). Lilitumiwa katika tafsiri ya Kigiriki ya Biblia kwa kutafsiri neno la Kiebrania "Bustani ya Edeni" (גן עדן Gan Eden)[1]
Katika Agano la Kale
Katika Kiebrania פרדס (pardes) inapatikana mara tatu katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania): Wimbo Ulio Bora 4:13, Mhubiri 2:5 na Nehemia 2:8.
Katika Agano Jipya
Katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo neno linapatikana vilevile mara tatu: Luka 23:43 (Yesu msalabani alilitumia akimjibu mhalifu aliyetubu ili kumhakikishia watakuwa pamoja), 2 Kor 12:4 (Mtume Paulo alilitumia kuelezea hali ya pekee aliyojaliwa kwa njozi, Ufunuo 2:7 (kuhusiana na Kitabu cha Mwanzo 2:8 na mti wa uzima.
Katika Uislamu
Kwa Kiarabu na katika Quran inaitwa فردوس., firdaus.
Tazama pia
- Dilmun
- Eridu
- El Dorado
- Goloka
- Nirvana
- Shangri-La
- Valhalla
Tanbihi
- ↑ Mwa 2:8: "Mwenyezi-Mungu akapanda bustani huko Edeni, upande wa mashariki, na humo akamweka huyo mwanamume aliyemuumba"
Viungo vya nje
- Etymology of "paradise", Balashon.com
- Etymology OnLine, etymonline.com
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |