Programufidia
Programufidia (kwa Kiingereza ransomware) ni aina ya programu haramu ambayo inakuzuia kutumia kompyuta yako hadi pale utakapolipa fidia kwa watu waliokutumia programu hiyo. Fidia mara nyingi hulipwa kwa kutumia sarafu dijitali kama vile Sarafu za Bit au Ukash.
Mashambulizi ya programufidia mara nyingi hufanyika kwa kutumia proramu ya Trojan ambayo inajifanya kuwa kama faili halali ambalo linamhadaa mtumiaji kompyuta kupakua au kufungua linapokuja kama kiambatanisho cha barua pepe. Hata hivyo, mfano mmoja wa teknolojia ya juu kabisa ya utapeli huu, "WannaCry worm", ilisafiri moja kwa moja kati ya kompyuta na kompyuta bila kuhitaji mtumiaji kufanya chochote.
Kuanzia mwaka wa 2012 matumizi ya programu hii yameongezeka kimataifa. [1] Kwa mfano, Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) linasema kuwa Programufidia aina ya CryptoWall ilivuna zaidi ya dola za Kimarekani milioni 18 hadi Juni 2015 kutokana na fidia za waathiriwa. [2]
Marejeo
- ↑ "Kuenea kwa programufidia". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-07-02. Iliwekwa mnamo 2017-10-16.
- ↑ "Ripoti ya FBI".
Viungo vya Nje
- Tovuti ya mradi wa kimataifa wa kupinga programufidia
- Historia ya Programufidia
- Habari kuhusu kuongezeka kwa mashambulizi ya Programufidia kutoka FBI
- Juu ya Programufidia
- Jinsi ya kulinda programu ya kuhifadhi tovuti ya Linux dhidi ya Programufidia
- Makala kuhusu iinsi ya kujilinda dhidi ya Programufidia
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |