Unguja Ukuu
Unguja Ukuu ni eneo la kiakolojia kwenye kisiwa cha Unguja , takriban kilomita 25 kusini -mashariki mwa Jiji la Zanzibar , ndani ya kata ya Unguja Ukuu Kaepwani . Utafiti wa wanaakiolojia (Chittick 1966; Juma 2004) ulionyesha kwamba huko kulikuwa na kituo cha biashara ya kimataifa mnamo mwaka 800 BK .
Kati ya mabaki yaliyogunduliwa kuna vyungu kutoka Ghuba ya Uajemi , pamoja na vipande vya vyungu vya China na vilulu kutoka Sri Lanka [ 1] . Kuna pia mabaki ya jengo la mawe kutoka enzi ya mnamo mwaka 900 linaloaminiwa kuwa msikiti [ 2] .
Tazama pia
Marejeo
↑ Mark Horton na Felix Chami: Swahili origins, uk. 141 katika "The Swahili World", Routledge 2018, ISBN: 978-1-138-91346-2
↑ Horton & Chami: Swahili origins, uk. 143 "A substantial stone building – possibly a mosque – was built at Unguja Ukuu at this time (Juma 2004). "
6°17′55″S 39°21′29″E / 6.2987°S 39.3580°E / -6.2987; 39.3580
The article is a derivative under the Creative Commons Attribution-ShareAlike License .
A link to the original article can be found here and attribution parties here
By using this site, you agree to the Terms of Use . Gpedia ® is a registered trademark of the Cyberajah Pty Ltd