Utetezi wa Ukristo
Utetezi wa Ukristo ni sehemu ya teolojia ya Ukristo inayolenga kutoa hoja za kutetea imani kwa Yesu Kristo dhidi ya zile za watu wa dini nyingine na za wale wasio na dini yoyote.
Kwa utetezi wa namna hiyo katika lugha nyingi limetoholewa neno la Kigiriki ἀπολογία, apologia, "utetezi wa sauti, hotuba ya utetezi"[1].
Ni tofauti kidogo na hoja zinaotumiwa na Wakristo dhidi ya dini na itikadi nyingine[2][3].
Historia
Utetezi wa Ukristo ulihitajika mapema dhidi ya hoja za Wayahudi na wengineo, hivyo unajitokeza katika Agano Jipya lenyewe, kwa mfano katika nyaraka za Mtume Paulo.
Baadaye uliendelea katika maandishi ya Mababu wa Kanisa kama vile Yustino mfiadini, Tertullianus, Origen na Agostino wa Hippo. Baadhi yao walitetea Ukristo dhidi ya dhuluma za serikali ya Dola la Roma na kwa hiyo wanaitwa Mababu watetezi (wa imani).
Baadaye kazi hiyo iliendelezwa na walimu wa Kanisa wa Karne za Kati, kama vile Anselm wa Canterbury, Thoma wa Akwino na wengineo wa Teolojia ya shule.
Wakati wa Falsafa ya mwangaza kati ya watetezi wa Ukristo dhidi ya falsafa hiyo anakumbukwa hasa Blaise Pascal na katika karne za mwisho Gilbert K. Chesterton.
Mbinu
Watetezi hao na wengineo wametumia hoja za kifalsafa, za kihistoria na za fani nyingine, mbali ya madondoo ya Biblia, kadiri ya hoja zilizotumiwa na wapinzani, ambao pengine wanakanusha mafundisho ya imani na maadili, pengine wanalaumu zaidi matendo ya wanakanisa, hasa viongozi.
Jambo lililoeleweka hasa kuanzia karne ya 20 ni kwamba mafarakano kati ya madhehebu ya wafuasi wa Kristo ndilo kwazo kubwa linalozuia watu wasimuamini Yesu, kama mwenyewe alivyoonyesha akisali wakati wa kwenda kuuawa: "Baba, wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja: mimi ndani mwako, nawe ndani mwangu, nao wakamilike katika umoja; ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ndiwe uliyenituma" (Yoh 17:22-23).
Ndiyo sababu juhudi za ekumeni ni sehemu muhimu ya utetezi wa Ukristo leo.
Maelekezo ya kisasa
"Tunahitaji utetezi wa aina mpya, kulingana na madai ya leo, ambayo izingatie kwamba jukumu letu si kushinda hoja, bali kuokoa watu, ni kuwajibika katika mapambano ya kiroho, si katika mabishano ya nadharia, ni kutetea na kukuza Injili, si sisi wenyewe".[4]
Tanbihi
- ↑ "ἀπολογία". Blue Letter Bible-Lexicon. Iliwekwa mnamo 7 Mei 2012.
{cite web}
: Cite has empty unknown parameter:|unused_data=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kahlos, Maijastina (2007). Debate and Dialogue : Christian and Pagan Cultures c. 360-430. Aldershot: Ashgate. ku. 7–9. ISBN 0-7546-5713-2.
- ↑ Ernestine, van der Wall (2004). "Ways of Polemicizing: The Power of Tradition in Christian Polemics". Katika T L Hettema and A van der Kooij (mhr.). Religious Polemics in Context. Assen: Royal Van Gorcum. ISBN 90-232-4133-9.
- ↑ Papa Yohane Paulo II, hotuba kwa Maaskofu wa Karibi, 7 Mei 2002
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Utetezi wa Ukristo kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |