Fritz Pregl

Fritz Pregl

Fritz Pregl (3 Septemba 1869 huko Laibach (leo Lubljana - Slovenia) - 13 Desemba 1930 Graz – Austria) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Austria. Aligundua mbinu za umikrokemia yaani uchambuzi wa kikemia penye kiasi cha dutu kidogo sana jinsi ilivyo mara nyingi katika uchambuzi wa sampuli za seli au viowevu vya kibinadamu kwenye maabara ya hospitali. Mwaka wa 1923 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fritz Pregl kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.