Gilgamesh
Gilgamesh alikuwa mfalme wa tano wa mji wa Uruk uliokuwa mji muhimu wa Wasumeri kusini mwa Mesopotamia ya kale. Baba yake Lugalbanda alikuwa mfalme wa tatu wa mji huu. Gilgamesh alitawala mnamo mwaka 2600 KK.
Gilgamesh alijenga ukuta uliozungusha mji wa Uruk. Ukuta huo ulikuwa ulinzi mwema na ndani yake mji uliendelea kuwa kitovu cha uchumi katika Mesopotamia.
Jina lake linafahamika hasa kutokana na Utenzi wa Gilgamesh ambao ni kati ya mifano ya kwanza kabisa ya fasihi andishi. Kufuatana na shairi hilo alikuwa theluthi moja binadamu na theluthi mbili mungu.[1]
Tanbihi
- ↑ Osborn, Kevin; Dana Burgess (1998). The Complete Idiot's Guide to Classical Mythology. Alpha Books. p. 30. ISBN 0028623851.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gilgamesh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |