Mkoa wa Kasai Mashariki
Mkoa wa Kasai Mashariki | |
Majiranukta: 06°09′S 23°36′E / 6.150°S 23.600°E | |
Nchi | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
---|---|
Makao makuu | Mbuji-Mayi |
Serikali | |
- Gavana | Dominique Nkangu Kabengela |
Eneo | |
- Jumla | 9,545 km² |
Idadi ya wakazi (2020 est.) | |
- Wakazi kwa ujumla | 3,864,3,000 |
National language | Tshiluba |
Tovuti: kasaiest.cd |
Kasai Mashariki (Kasai-Oriental kwa Kifaransa) ni mmojawapo kati ya mikoa 26 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kasai-Oriental ni kati ya maeneo duniani yenye almasi nyingi.
Makao makuu ya mkoa ni Mbuji-Mayi.
Jina la mkoa linatokana na mto Kasai.
Historia
Kasai-Oriental inakaliwa hasa na Waluba. Kabla ya ukoloni sehemu kubwa za mkoa zilkuwa chini ya milki ya Luba.
Wakati wa uhuru wa Kongo wanasiasa wa sehemu hii walijaribu kuanzisha dola la kujitegemea la Kasai kusini lakini jeshi la serikali kuu lilivamia eneo lake. Baada ya vita ya miezi minne iliyokuwa na wahanga kwa maelfu eneo lilirudishwa Kongo na kugawiwa.
Lugha
Kifaransa ni lugha rasmi. Tshiluba ni lugha inayotumiwa na wakazi wengi na ni moja ya lugha za kitaifa za Kongo.
Almasi
Eneo la mji wa Mbuji-Mayi linazalisha asilimia 10 ya almasi zote zinazotolewa duniani. Uchimbaji unasimamiwa na kampuni ya Société Minière de Bakwanga, ingawa wananchi wengine wanajaribu kuchimba almasi kibinafsi. Kwa jumla wakazi wa mkoa hawafaidiki na utajiri huo.
Marejeo
Équateur | Ituri | Kasai | Kasai Kati | Kasai Mashariki | Katanga Juu | Kinshasa | Kivu Kaskazini | Kivu Kusini | Kongo Kati | Kwango | Kwilu | Lomami | Lomami Juu | Lualaba | Mai-Ndombe | Maniema | Mongala | Sankuru | Tanganyika | Tshopo | Tshuapa | Ubangi Kaskazini | Ubangi Kusini | Uele Chini | Uele Juu | |
+/- |
Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Kasai Mashariki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |