Italia

Jamuhuri ya Italia
Repubblica Italiana (Kiitalia)
Wimbo wa taifa
"Il Canto degli Italiani"(Kiitalia)
"Wimbo wa Waitalia"

ukubwa_wa_picha

Eneo la Italia katika bara la Ulaya

Jiji kubwa
(na Mji Mkuu)
Roma
Lugha rasmi Kiitalia
Kabila
  • 91.0% Waiitalia
  • 9.0% Wengine
Dini
Utaifa Miitalia
Aina ya Serikali Jamhuri ya Muungano wa Rais
Rais Sergio Mattarella
Waziri Mkuu Giorgia Meloni
Rais wa Seneti Ignazio La Russa
Historia
Muungano 17 Machi 1861
Jamuhuri 12 Juni 1946
Katiba ya sasa 1 Januari 1948
Ukubwa wa eneo
Jumla 301,340 km²
Asilimia ya Maji 1.24 %
Idadi ya Watu
Mwaka wa Makisio
Idadi ya watu (makisio) increase 58,968,501
Pato la Taifa PPP
Mwaka wa Makisio 2024
Jumla increase $3.597 Trilioni [1] (ya 13)
Capita increase $60,992 [1]
Pato la Taifa
Mwaka wa Makisio 2024
Jumla increase $2.376 Trilioni [1] (ya 8)
Capita increase $40,286 [1]
Kiashiria cha Maendeleo ya Watu (2022) increase 0.906 [2] (28)
Maendeleo ya Juu Sana
Kiashiria cha ukosefu wa usawa (2021)
34.8
Ukosefu wa usawa wa kati
Sarafu Euro EU
Eneo la saa UTC+1 (CET)
Nambari ya mwito +39
Upande wa Gari Kulia
Intaneti TLD .it


Italia, rasmi Jamhuri ya Italia, ni nchi iliyopo Kusini mwa Ulaya. Inapakana na Ufaransa upande wa magharibi, Uswisi na Austria upande wa kaskazini, na Slovenia upande wa mashariki. Nchi hii ina idadi ya watu takriban milioni 60 na ina eneo la kilomita za mraba 301,340. Roma, jiji kubwa zaidi, pia ni mji mkuu. Italia imegawanywa katika mikoa 20 na inajulikana kwa alama zake za kihistoria, sanaa, vyakula, na kama mahali pa kuzaliwa kwa Dola la Kirumi na Renaissance.

Jiografia

Umbo la jamhuri, kama lile la rasi yake, linafanana na mguu linalozungukwa na maji ya Mediteraneo pande tatu.

Milima ya Appennini inaunda uti wa mgongo wake, wakati ile ya Alpi, ambayo ni mirefu zaidi, inaunda kwa kiasi kikubwa mpaka kati ya Italia na nchi nyingine za Ulaya.

Mlima mrefu zaidi, ukiwa na mita 4,810 juu ya usawa wa bahari, unaitwa Monte Bianco (Mlima Mweupe) na uko mpakani kwa Ufaransa.

Visiwa viwili vikubwa vya Sisilia na Sardinia ni sehemu za Italia pamoja na visiwa vingi vidogovidogo, vile vya Pelagie vikiwa upande wa Afrika.

Italia ina volkeno 14, ambazo 4 kati yake ziko hai: ile ndefu zaidi kuliko zote za Ulaya (mita 3,329) inaitwa Etna na iko mashariki mwa Sisilia. Italia inaongoza Ulaya kwa wingi wa matetemeko ya ardhi.

Mto mrefu zaidi unaitwa Po na una urefu wa kilomita 652. Mito mingine mirefu ni Adige, Tevere, Adda, Oglio, Tanaro, Ticino, Arno, Piave, Reno, Sarca-Mincio n.k.

Maziwa makubwa zaidi ni: Garda (km2 367.94), Ziwa Maggiore (212.51, likiingia Uswisi), Ziwa la Como (145.9), Trasimeno (124.29) na Ziwa la Bolsena (113.55).

Kutokana na urefu mkubwa wa Italia toka kaskazini hadi kusini, hali ya hewa ni tofauti sana, kuanzia baridi kali sana hadi joto kali sana.

Mikoa

Bendera Jina Makao makuu Eneo (km2) Wakazi Msongamano wa watu/km² Wilaya Miji Miji mikubwa Hali ya utawala
Abruzzo L'Aquila 10,763 1,307,919 122 4 305 - Kawaida
Bonde la Aosta Aosta 3,263 126,933 39 0 74 - Kujitawala
Puglia Bari 19,358 4,045,949 209 6 258 Bari Kawaida
Basilicata Potenza 9,995 575,902 58 2 131 - Kawaida
Calabria Catanzaro 15,081 1,954,403 130 5 409 Reggio Calabria Kawaida
Campania Napoli 13,590 5,761,155 424 5 551 Napoli Kawaida
Emilia-Romagna Bologna 22,446 4,354,450 194 9 348 Bologna Kawaida
Friuli-Venezia Giulia Trieste 7,858 1,219,356 155 4 218 Trieste Kujitawala
Lazio Rome 17,236 5,550,459 322 5 378 Rome Kawaida
Liguria Genoa 5,422 1,565,349 289 4 235 Genoa Kawaida
Lombardia Milan 23,861 9,749,593 409 12 1544 Milan Kawaida
Marche Ancona 9,366 1,541,692 165 5 239 - Kawaida
Molise Campobasso 4,438 312,394 70 2 136 - Kawaida
Piemonte Turin 25,402 4,366,251 172 8 1206 Turin Kawaida
Sardinia Cagliari 24,090 1,637,193 68 8 377 Cagliari Kujitawala
Sisilia Palermo 25,711 4,994,817 194 9 390 Catania, Messina, Palermo Kujitawala
Trentino-Alto Adige/Südtirol Trento 13,607 1,036,707 76 2 333 - Kujitawala
Toscana Firenze 22,994 3,679,027 160 10 287 Firenze Kawaida
Umbria Perugia 8,456 885,535 105 2 92 - Kawaida
Veneto Venisi 18,399 4,865,380 264 7 581 Venisi Kawaida

Historia

Makala kuu: Historia ya Italia
Mji wa Venisi, uliojengwa juu ya visiwa 117.
Mnara wa Pisa, pamoja na kanisa kuu la Pisa na batizio yake.
Ikulu ya Caserta.

Akiolojia imethibitisha uwepo wa Homo neanderthaliensis miaka 128,000-187,000 hivi iliyopita. Homo sapiens sapiens alifika miaka 40,000 hivi iliyopita.

Kufikia milenia ya 1 KK wakazi wengi walikuwa wa jamii ya Kizungu na kutumia lugha za Kihindi-Kiulaya.

Peninsula ya Italia iliunganishwa mara ya kwanza na Jamhuri ya Roma (509-27 KK), lakini hiyo ilipoenea Ulaya kusini na magharibi, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi ikawa na sura ya kimataifa kama Dola la Roma.

Umoja ulipotea kuanzia uvamizi wa jiji la Roma uliofanywa na Wagermanik (476 BK) na hasa baada ya ufalme wa Karolo Mkuu aliyetawala sehemu ya kaskazini tu.

Juhudi za kuurudisha umoja zilifanywa hasa katika karne ya 19, ambapo Ufalme wa Sardinia uliteka sehemu kubwa ya Italia (hasa miaka 1860, 1866 na 1870) na kubadilika kuwa Ufalme wa Italia wenye makao makuu Roma.

Baada ya vita vikuu vya pili iligeuka Jamhuri yenye katiba inayotia mamlaka kuu mikononi mwa bunge.

Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957 ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa pesa ya pamoja (Euro).

Maendeleo

Italia ni kati ya nchi zilizoendelea, ikiwa na nafasi ya nane kwa nguvu ya uchumi duniani, hivyo ni mwanachama wa G7, G8 na G20.

Sanaa na utalii

Kuanzia kushoto kwa kufuata mzunguko wa mishale katika saa: Kanisa kuu la Florence, lenye kuba la matofali kubwa kuliko yote duniani;[3][4] Basilika la Mt. Petro, kanisa kubwa kuliko yote duniani, liko Vatikani, nchi inayozungukwa na Italia pande zote;[5] kanisa kuu la Milano, la tano duniani kwa ukubwa;[6] na Basilika la Mt. Marko, Venezia.[7]

Italia ndiyo nchi inayongoza duniani kwa kuwa na mahali pengi (51) pa kimaumbile na pa kihistoria palipoingizwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".

Kwa sababu hiyo pia inashika nafasi ya 5 kati ya nchi zote zilizo lengo la utalii.

Watu

Wananchi wana sifa za pekee kati ya Wazungu wote, hata upande wa DNA, kutokana na jiografia na historia ya rasi.

Ni kati ya nchi ambamo watu wanatarajiwa kuishi miaka mingi zaidi, lakini pia ni kati ya nchi ambapo uzazi ni mdogo zaidi: wanaokufa ni wengi kuliko wanaozaliwa.

Kutokana na umati wa Waitalia waliohama nchi hiyo karne za nyuma, sasa zaidi ya watu milioni 60 nje ya Italia wana asili ya nchi hiyo, mbali na raia zaidi ya milioni 4 wanaoishi nje.

Lugha rasmi ni Kiitalia, inayotegemea zaidi lahaja za Italia ya Kati, lakini siku hizi inatumiwa na wananchi walio wengi hata katika mikoa mingine, ambayo kwa jumla ni 20.

Upande wa dini, wengi wao (81.2%) ni Wakristo wa Kanisa Katoliki, wakifuatwa na Waorthodoksi (2.8%, wengi wao wakiwa wahamiaji, hasa kutoka Romania) na Waprotestanti (1.1%, wengi wao wakiwa Wapentekoste). Uhamiaji mwingi wa miaka ya mwisho wa karne ya 20 umeleta pia Uislamu (3.7%) na dini nyingine.

Dini zote zinaachiwa uhuru na, tofauti na nchi nyingi za Ulaya, waumini wake wanajitahidi kiasi kufuata ibada (29% kila wiki).

Watu maarufu

Tazama pia

Tanbihi

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Italy GDP profile". Iliwekwa mnamo 2025-01-30.
  2. "Italy Hdi". Iliwekwa mnamo 2025-01-31.
  3. "The Duomo of Florence | Tripleman". tripleman.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-06. Iliwekwa mnamo 25 Machi 2010.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Brunelleschi's Dome". Brunelleschi's Dome.com. Iliwekwa mnamo 25 Machi 2010.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "St. Peter's Basilica (Basilica di San Pietro) in Rome, Italy". reidsitaly.com.
  6. See List of largest church buildings in the world; note that the #3 entry, First Family Church building in Kansas, is now a school education complex.
  7. "Basilica di San Marco". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-05. Iliwekwa mnamo 10 Februari 2016. {cite web}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Italia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.