Nabii Yona

Nabii Yona alivyochorwa na Michelangelo katika dari la Kikanisa cha Sisto IV, Vatikano.

Yona (kwa Kiebrania: יוֹנָה, Yônā; kwa Kiarabu: يونس, Yūnus, Yūnis au يونان, Yūnān ; kwa Kilatini: Ionas; alifariki 761 KK hivi) ni jina la nabii wa Israeli aliyeishi katika karne ya 8 KK.

Pia ni jina la mhusika mkuu wa kitabu cha Yona katika Biblia ya Kiebrania (Tanakh) na hivyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo. Kutokana na hadithi hiyo, Yona anazungumziwa pia katika Injili na katika Kurani.

Hasa simulizi maarufu la yeye kutoka salama katika tumbo la mnyama mkubwa wa baharini limetumiwa na Yesu kama kidokezo cha ufufuko wake mwenyewe [1]

Wakatoliki wanamheshimu kama mtakatifu na kuadhimisha sikukuu yake tarehe 21 Septemba[2][3].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Yona kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.