Primasia

Mkusanyiko wa Mitume Thenashara. Picha takatifu ya karne ya 14, Moscow, Russia.


Primasia (kwa Kiingereza "Primacy", kutokana na Kilatini "Primus", yaani "wa kwanza") ni msamiati wa teolojia ya Ukristo ambao unajaribu kueleza kwa nini baadhi ya maaskofu wana mamlaka juu ya wenzao, hasa Papa wa Roma kuwa na mamlaka juu ya maaskofu wote wa Kanisa Katoliki.

Uwepo wa mamlaka ya namna hiyo unakubaliwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Wakatoliki wa Kale na Waanglikana, ambao wote wana maaskofu wakuu na hata Mapatriarki wenye mamlaka juu ya maaskofu wakuu.

Tofauti zinajitokeza katika kueleza asili na utekelezaji wake unaotakiwa kuendana na usinodi.

Kwa Wakatoliki, primasia ilitakwa na Yesu mwenyewe katika kuchagua mitume wake pamoja na mkuu wao, Simoni Petro, ambaye katika orodha zao zote nne zilizomo katika Agano Jipya anawatangulia wenzake, tena Injili ya Mathayo 10:1-4 inasema wazi kwamba ndiye "wa kwanza".

Madondoo mengine yanayotumiwa na Wakatoliki kama uthibitisho ni Math 16:17‑19 Lk 22:32 na Yoh 21:15‑17.

Tanbihi

Marejeo

Vyanzo

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Primasia kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.