Ujio wa pili
Ujio wa pili ni imani ya kwamba Yesu, aliyekuja mara ya kwanza kwa unyenyekevu alipozaliwa na Bikira Maria, atashuka tena toka mbinguni kwa utukufu siku ya kiyama.
Katika Ukristo
Msingi wa tumaini hilo katika Ukristo ni ahadi alizotoa mwenyewe na ambazo zinasomwa katika Injili (Math 24:27; 25:31; Lk 17:30; Yoh 6:39-40).
Ufafanuzi zaidi ulitolewa na Mtume Paulo (Mdo 10:42; 17:31; Rom 2:5-16; 14:10; 1Kor 4:5; 15:23; 2Kor 5:10; Fil 1:6; 1Tim 6:14; 2 Tim 4:1,8; Tito 2:13; 1Thes 5:2; 2Thes 1:5; 2:1-9) na wengineo katika vitabu vingine vya Agano Jipya (1Pet 4:13; Yak 5:7) na baadaye.
Katika Agano Jipya neno ἐπιφάνεια, epiphaneia, kutokea, limetumika mara 5 kuhusiana na kurudi kwa Kristo,[1] kumbe neno παρουσία, parousia, kufika au kuwepo, mara 17.[2][3]
Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli (karne ya 4) ilikiri kwamba "atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho".
Hata hivyo Wakristo wanatofautiana kuhusu jambo hilo kadiri ya madhehebu yao, lakini pia kadiri ya rai binafsi kuhusu maana halisi ya maneno yake.
Kama Yesu mwenyewe alivyotabiri, jambo hilo litaleta udanganyifu mwingi ambao alitaka wafuasi wake wajihadari usiwapate.
Kweli karne hata karne walitokea watu kutabiri mwaka au hata tarehe ya tukio hilo; tena wengine walisema limeshafanyika, kumbe bado.
Yesu alisema, "Hakuna anayejua siku wala saa". Lakini watu hao walijaribu kutumia namba za Biblia ili kuhesabu itakuwa lini.
Katika Uislamu
Katika Islam, عيسى (ʿĪsā, Isa) anaheshimiwa kama mtume na Masihi aliyetumwa kwa Waisraeli (banī isrā'īl) akiwaletea kitabu kipya, Injili.[4]
Quran inazungumzia ujio wa pili wa huyo Yesu katika sura Az-zukhruf (43:61) kama ishara ya siku ya hukumu.[5][6]
Pia kuna Hadithi za Mtume Muhammad zinazotabiri wazi ujio wake.[7][8]
Tanbihi
- ↑ NT usage
- ↑ "Strong's G3952". Blueletterbible.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-10. Iliwekwa mnamo 2009-11-21.
- ↑ "CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: General Judgment (Last Judgment)". Newadvent.org. 1910-10-01. Iliwekwa mnamo 2009-11-21.
- ↑ The Oxford Dictionary of Islam, p.158
- ↑ Yusuf Ali, Abdullah. "Surah Az-zukhruf". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-15. Iliwekwa mnamo 2014-09-02.
- ↑ kathir, Ibn. "Tafsir al-Qur'an al-Azim".
- ↑ "Isa", Encyclopedia of Islam
- ↑ Sonn (2004) p. 209
Marejeo
- Explanatory text in The New Jerusalem Bible (1990). Doubleday. ISBN 0-385-14264-1
- Max Heindel. How Shall We Know Christ at His Coming?, May 1913 (stenographic report of a lecture, Los Angeles), ISBN 0-911274-64-2
- C. S. Lewis. (1960). The World's Last Night and Other Essays. Harcourt Brace Jovanovich. ISBN 0-15-698360-5
- Markus Mühling. Grundinformation Eschatologie. Systematische Theologie aus der Perspektive der Hoffnung, Vandenhoeck & Ruprecht, Göttingen 2007, ISBN 978-3-525-03619-8, 221–241
- James Stuart Russell. The Parousia, A Careful Look at the New Testament Doctrine of the Lord's Second Coming
- Emanuel Swedenborg. The Consummation of the Age; the Coming of the Lord; and the New Heaven and New Church, Chapter 14 in The True Christian Religion Containing the Universal Theology of The New Church Foretold by the Lord in Daniel 7; 13, 14; and in Revelation 21; 1,2 (Swedenborg Foundation 1952)
- Paramahansa Yogananda. The Second Coming of Christ: The Resurrection of the Christ Within You. Self-Realization Fellowship, 2004. ISBN 978-0876125557
Viungo vya nje
- "Lecture XV: On the Clause, And Shall Come in Glory to Judge the Quick and the Dead; Of Whose Kingdom There Shall Be No End.", delivered by Cyril of Jerusalem in the mid-4th century.
- "The Second Coming.", a summary article.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ujio wa pili kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |