Zimbabwe
| |||||
Kaulimbiu ya Taifa Unity, Freedom, Work (Kiingereza: Umoja, Uhuru, Kazi) " | | |||||
Wimbo wa Taifa | |||||
Location of Zimbabwe | |||||
Lugha rasmi | Kiingereza na 15 nyingine | ||||
Mji Mkuu | Harare | ||||
Mji mkubwa | Harare | ||||
Rais | Emmerson Mnangagwa | ||||
Eneo - Jumla -Maji -Eneo kadiriwa |
km² 390,757 1% ya 60 duniani | ||||
Umma - Kadirio - Sensa, - Msongamano wa watu |
15,178,979 ya 66 duniani (2022) ; 32/km² ; ya duniani | ||||
Chumo cha uchumi - Jumla - kwa kipimo cha umma |
$24.99 billion (Orotha ya nchi GDP (kidogo)) $2,100 (Orodha ya nchi kulingana na GDP kwa umma) | ||||
Uhuru - Kadirifu - Barabara |
(kama Rhodesia) 11 Novemba 1965 (kama Zimbabwe) 18 Aprili 1980 | ||||
Fedha | Dolar ya Marekani| | ||||
Saa za Eneo | UTC +2 | ||||
Intaneti TLD | .zw | ||||
kodi za simu | 263 |
Jamhuri ya Zimbabwe (iliyojulikana wakati wa ukoloni kama Rhodesia ya Kusini) ni nchi isiyo na bahari iliyoko upande wa kusini wa Bara la Afrika, kati ya mto Zambezi na mto Limpopo.
Imepakana na Afrika ya Kusini upande wa kusini, Botswana upande wa magharibi, Zambia upande wa kaskazini-mashariki, na Msumbiji upande wa mashariki.
Jina
Jina Zimbabwe linatokana na neno "dzimba dzamabwe" linalomaanisha "nyumba ya mawe" kwa lugha ya Kishona. Nyumba hiyo ya mawe, ambayo imehifadhiwa kama eneo la kihistoria, ilikuwa makao ya Ufalme wa Mutapa ambaye mfalme wake aliongoza eneo hilo miaka ya kale.
Eneo
Zimbabwe imegawiwa katika mikoa 8 na miji 2 yenye hadhi ya mikoa. Imegawiwa zaidi katika wilaya 59 na kata 1,200.
- Bulawayo (mji),
- Harare (mji),
- Manicaland,
- Mashonaland ya Kati,
- Mashonaland Mashariki,
- Mashonaland Magharibi,
- Masvingo,
- Matabeleland Kaskazini,
- Matabeleland Kusini na
- Midlands.
Miji minne mikubwa ya Zimbabwe ni:
- Bulawayo, mji wa pili kwa ukubwa
- Harare, mji mkuu
- Chitungwiza
- Mutare
Historia
Historia ya awali
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
Tangu karne ya 11, Zimbabwe ya leo imekuwa na falme imara kwenye njia muhimu ya biashara, hasa ufalme wa Mutapa.
Ukoloni
Kampuni ya British South Africa ya Cecil Rhodes iliweka mipaka ya sasa katika miaka ya 1890.
Koloni la Uingereza lilianzishwa mwaka 1923 kwa jina la Southern Rhodesia.
Mwaka 1965, serikali ya walowezi Wazungu ilijitangazia uhuru kwa jina la Rhodesia tu.
Baada ya miaka 14 ya kutengwa kimataifa na kupigana na raia Waafrika katika miaka ya 1970, mapatano ya mwaka 1979 yalikubali wakazi wote wawe na haki ya kupiga kura na nchi ikawa huru kweli kwa jina la Zimbabwe mwaka 1980.
Baada ya uhuru
Rais Robert Mugabe alipata umaarufu katika siasa kama mpiganaji dhidi ya ukoloni lakini pia kama aina ya dikteta aliyerudisha nyuma uchumi wa nchi.
Baada ya yeye kulazimishwa na wanajeshi kujiuzulu, tarehe 24 Novemba 2017 Emmerson Mnangagwa amekuwa rais mpya wa Zimbabwe.
Watu
Wakazi wengi (82%) ni wa kabila la Washona, 14% ni Wandebele, 2% ni wa makabila mengine ya Kiafrika, 1% ni machotara, Wahindi, Wazungu n.k.
Kwa sasa lugha rasmi ni 16. Lugha kubwa ni Kishona (70%) na Kindebele (20%). Kiingereza ni lugha ya kwanza ya chini ya asilimia 2.5% za wakazi.
Upande wa dini, 84.1% ni Wakristo (hasa Waanglikana, Wakatoliki 8%, Wasabato na Wamethodisti). Waliobaki ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika (4.5%), ni Waislamu (0.7%), au hawana dini (10.2%) .
Mawasiliano
Mawasiliano ya simu na mitambo yake yanaendeshwa na Tel-One0, kampuni ya serikali.
Kuna kampuni 3 za simu za mikononi: Econet Wireless, Net*One na Telecel.
Tazama pia
- Wilaya za Zimbabwe
- Kata za Zimbabwe
- Orodha ya miji ya Zimbabwe
- Mawasiliano Zimbabwe
- Utamaduni wa Zimbabwe
- Orodha ya lugha za Zimbabwe
- Muziki wa Zimbabwe
- Waandishi wa Zimbabwe
- Mambo ya kigeni Zimbabwe
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Tanbihi
Viungo vya nje
Serikali
- [1] Archived 16 Machi 2016 at the Wayback Machine. Tovuti rasmi ya Bunge la Zimbabwe
- [2] Archived 24 Oktoba 2008 at the Wayback Machine. Tovuti rasmi ya serikalimirror site
Habari
- Ardhi na siasa Archived 15 Mei 2006 at the Wayback Machine.-BBC usanifu wa utekelezaji wa arthi.
- [3] Zimbabwe destruction: (hadithi ya mtu mmoja)
- New Zimbabwe UK-Based independent daily newspaper
- AllAfrica.com - Zimbabwe news headline links
- IFEX - Zimbabwe Archived 27 Juni 2006 at the Wayback Machine. press freedom violations
- The Sunday Mirror Archived 15 Juni 2006 at the Wayback Machine. weekly newspaper
- Zimbabwe Independent weekly newspaper
- The Zimbabwean UK-based independent weekly newspaper (gazeti ya wiingereza)
- The Herald State-owned daily newspaper
- Zimbabwe Situation A comprehensive collection of news stories concerning Zimbabwe from different sources
- Haikona! Zimbabwe News Blog Archived 17 Aprili 2006 at the Wayback Machine. Taarifa ya habari Zimbabwe
Wanamgambo
Maelekezo
- (Chuo kikuu cha kolombia - Zimbabwe maelekezo ya WWW-VL
- Open Directory Project - Zimbabwe maelekezo
- Stanford University - Afrika kusini mwa Sahara: Zimbabwe maelekezo
- Yahoo! - Zimbabwe Archived 6 Januari 2009 at the Wayback Machine. maelekezo
Utalii
- Travel Overview of Zimbabwe Archived 9 Julai 2006 at the Wayback Machine.
- Facts about Zimbabwe Archived 27 Aprili 2006 at the Wayback Machine.
Nyingine
- Amnesty International (Zimbabwe) Archived 16 Juni 2006 at the Wayback Machine.
- Dariro (makala ya kutafuta vifungu vya Zimbabwe)
- itsbho.com Leading Zimbabwean entertainment website Archived 29 Machi 2018 at the Wayback Machine.
- RSF report on Zimbabwe from 2003 Archived 21 Aprili 2005 at the Wayback Machine.
- Writers of Zimbabwe – (makala ya muadishi kwa waandishi wa Zimbabwe)
- Zimbabwe Human Rights NGO Forum-(haki za kibinadamu)
- ZIMBABWE Archived 10 Mei 2005 at the Wayback Machine. (viungo via taarifa)
- "Dead Capital" in Zimbabwe Archived 13 Agosti 2006 at the Wayback Machine.
- 5 year archive of Zimbabwe news updated daily
- Zimbabwe Crisis Habari za kuazua zilizo chapishwa wakati wa kura mnamo 2000.
- ZimFest Miziki ya Zimbabwe kila mwaka, Marekani kaskazini.
- Zimbabweb Archived 9 Januari 2014 at the Wayback Machine. lango la taarifa Zimbabwe
- zwnews Lango la habari Zimbabwe
- Economic Development Bulletin (Maelezo ya maedeleo ya uchumi) kupoteza haki ya mali Zimbabwe na udhoofu wa uchumi.
- Cato Journal Archived 2 Januari 2011 at the Wayback Machine. Kifungu cha kuanguka kwa nchi ya Zimbabwe
- Center for Global Development Archived 6 Aprili 2006 at the Wayback Machine. (senta ya maedeleo ya dunia) garama na mwanzo wa misukosuko Zimbabwe.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Zimbabwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |