Bahari ya Weddell

Mtazamo kutoka angani juu ya Antaktika. Bahari ya Weddell ndiyo 'bay' kwenye kona ya juu kushoto.
Barafu inayofunika sehemu ya kusini ya Bahari ya Weddell.
Siwa barafu.

Bahari ya Weddell ni sehemu ya Bahari ya Kusini iliyopo katika hori kubwa baina ya Rasi Antaktiki na Nchi ya Coats. Sehemu kubwa ya eneo lake imefunikwa na barafu ya kudumu. Upana kwenye mdomo wa hori ni karibu km 2,000, eneo hilo ni karibu kilomita za mraba milioni 2.8. Kina chake ni baina ya mita 500 hadi 5,000.

Bahari hiyo ilipewa jina la nahodha Mwingereza na mwindaji wa sili James Weddell aliyeingia katika bahari hiyo mnamo 1823 akafika hadi latitudo ya kusini ya 74. Sili wa Weddell ni moja ya wanyama ambao wanaishi katika eneo hilo.

Argentina (nchi iliyo karibu zaidi), Chile na Ufalme wa Muungano wanashindana kuhusu usimamizi wa sehemu hii.

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.