INRI

Mchoro wa Diego Velázquez, Yesu msulubiwa, 1631, Prado (Madrid, Hispania) unaonyesha anwani kichwani pake.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

INRI ni kifupisho cha maneno ya Kilatini "Iesus Nazarenus Rex Iudaeorum" ("Yesu Mnazareti Mfalme wa Wayahudi").

Ni kwamba, kadiri ya Injili zote nne, Ponsio Pilato, liwali wa Palestina, aliamua Yesu asulubiwe kulingana na shtaka la viongozi wa Wayahudi waliodai mtuhumiwa alijitangaza kuwa mfalme na kupinga mamlaka ya Kaisari wa Dola la Roma, kwa wakati huo Tiberius, ingawa Pilato alikuwa ametambua shtaka halikuwa la kweli, bali lilitokana na husuda.

Kadiri ya Injili ya Yohane (19:19-22), Pilato mwenyewe alisisitiza kwamba, katika maandishi yaliyotakiwa kuwajulisha watu sababu ya adhabu hiyo, iwekwe wazi kwamba Yesu aliuawa kama mfalme wa Wayahudi, ingawa neno hilo lilichukiza viongozi wa taifa.

Maneno ya ilani hiyo yaliandikwa katika lugha tatu:

  • Kilatini (Iesus Nazarenus Rex Iudaeorum),
  • Kigiriki (Ἰησοῦς ὁ Ναζωραῖος ὁ Bασιλεὺς τῶν Ἰουδαίω). Kutokana na herufi hizo, Wagiriki wanaandikwa INBI.
  • Kiebrania (ישוע הנוצרי ומלך היהודים). Herufi za kwanza za maneno hayo kwa Kiebrania ni יהוה, YHWH, ndilo jina takatifu la Mungu katika Biblia ya Kiebrania.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu INRI kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.