Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika.
Faili:Hallies.jpgHaile Selassie wa EthiopiaHaile Selassie (23 Julai, 1892 – 27 Agosti, 1975) alikuwa Kaisari au Negus Negeste wa Ethiopia. Alizaliwa katika kijiji kiitwacho Ejersa. Kabla ya kuwa mfalme aliitwa Ras Tafari Makonnen. Jina lake la kifalme lina maana ya "Utukufu wa Utatu (Mtakatifu)". Pia anafahamika kwa jina la Simba wa Yuda, Mfalme wa wafalme (H.I.M).Baba yake alikuwa mkabaila Mwethiopia aliyeitwa Ras Makonnen akawa gavana wa Harar, familia yake ina watoto 11. Alikuwa Mkristo muumini wa madhehebu ya Orthodoksi ya Ethiopia.
Jameson Hall na Jammie Plaza, mahali spesheli katika kampasi ya juuChuo Kikuu cha Cape Town (UCT) ni chuo kikuu cha umma kilicho mjini Cape Town katika jimbo la Rasi ya Magharibi la Afrika Kusini. UCT ilianzishwa mwaka wa 1829 kama South African College, na ndio chuo kikuu kongwe zaidi nchini Afrika Kusini. Kampasi kuu, inayojulikana kama Upper Campus, iko katika Rhodes Estate kwenye mteremko wa Devil's Peak. Kampasi hii ina, katika eneo lililopakiwa kiasi, na vitivo vya Sayansi, Uhandisi, Biashara, na Masomo ya Kibinadamu (isipokuwa idara za sanaa), vilevile Smuts Hall na makazi ya Fuller Hall. Upper Campus imejengwa kuzunguka Jameson Hall, eneo la mahafali na sherehe nyingine, vilevile mitihani mingi. Majengo ya awali na mpangilio wa Upper Campus uliundwa na JM Solomon na kujengwa kati ya 1928 na 1930. Tangu wakati huo, majengo mengi yameongezwa jinsi chuo kimezidi kukua. Upper Campus pia ni nyumbani kwa maktaba kuu iitwayo Chancelor Oppenheimer Library ambayo ina makala mengi ya Chuo Kikuu, kusanyiko la kama milioni 1.3.
...kwamba Ubuntu au "Obuntu" ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano wa jamii kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii. Neno ubuntu limetoka kwenye lugha za Kizulu na KiXhosa za Afrika Kusini. Neno la Kihaya "Obuntu" au kwaKiswahili "utu" linabeba, kwa kiasi fulani, maana ya neno Obuntu.