Skype

Nembo ya Skype
Nembo ya Skype

Skype (matamshi: / skaɪp /) ni programu ambayo inatumia intaneti kupiga simu za sauti na video kwa teknolojia inayoitwa Voice over Internet Protocol (VoIP). Skype huwezesha watumiaji kutuma ujumbe wa maneno, video, sauti, picha na kufanya mikutano kwa video.

Iliundwa mwaka 2003 na Mswidi na Mdenmark Niklas Zennström na Janus Friis wakishirikiana na Waestonia Ahti Heinla, Priit Kasesalu, na Jaan Tallinn, na kwa sasa inaendeshwa na kampuni ya huko Luxemburg inayoitwa Skype Technologies SARL, ambayo tangu mwaka k2011 ni sehemu ya Microsoft.

Kabla ya kumilikiwa na Microsoft, Skype ilimilikiwa na eBay kuanzia Septemba 2005 hadi 2011. eBay iliinunua kutoka kwa walioizindua kwa dola za Kimarekani bilioni 2.6 miaka 2 baada ya kuzinduliwa.[1] [2]

Mwaka wa 2009, eBay iliuzia Silver Lake, Andreessen Horowitz, na Bodi la Mipango ya Uwekezaji wa Pensheni la Kanada asilimia 65 ya hisa za Skype kwa kima cha dola za Kimarekani bilioni 1.9 wakati thamani ya Skype ilikuwa takriban dola za Kimarekani 2.75.

Tarehe 10 Mei 2011, Microsoft ilianza mipango ya kumiliki Skype Communications, S.à r.l kwa kima cha dola za Kimarekani bilioni 8.5 na tarehe 13 Oktoba mwaka huo mipango ya umiliki ikakamilika.[3][4]

Jina Skype linatokana na "Sky peer-to-peer" ambapo ilifupishwa kuwa "Skyper". Hata hivyo, anuani ya tovuti yenye jina hilo ilikuwa tayari imenunuliwa na kampuni nyingine,[5] hivyo herufu "r" iliondolewa na kuwa Skype.[6]

Marejeo

  1. "EBay to buy Skype in $2.6bn deal". BBC. 12 Septemba 2005. Iliwekwa mnamo 2 Oktoba 2014.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Canada Pension plan buys Skype stake | Toronto Star". Thestar.com. 2 Septemba 2014. Iliwekwa mnamo 21 Agosti 2014.{cite web}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Microsoft to Acquire Skype - About Skype". web.archive.org. 2011-05-12. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-12. Iliwekwa mnamo 2019-06-14.
  4. Toor Amar (2011-11-13). "Microsoft finalizes acquisition of Skype, Tony Bates shares his thoughts (video)". Engadget (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-06-14.
  5. "The World's Hottest VC?". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Januari 2008. {cite web}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  6. "Origin of the name/word Skype". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Novemba 2005. Iliwekwa mnamo 13 Agosti 2010. {cite web}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Skype kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.