Geoffrey Chaucer

Geoffrey Chaucer

Geoffrey Chaucer (mnamo 134325 Oktoba 1400) alikuwa mwandishi, mshairi na mwanafalsa Mwingereza. Ameitwa "Baba wa Fasihi ya Uingereza". kazio yake mashuhuri ni masimulizi ya "Canterbury Tales".

Chaucer alizaliwa mjini London katika familia ya wafanyabiashara wa divai. Habari za maisha yake kama mtoto na kijana ni chache. Alikuwa mwanajeshi katika vita ya Waingereza dhidi ya Ufaransa alipokamatwa 1360 akawa mfungwa kwa mudi mfupi. Kuna hati ya 1366 anaponekana kama balozi wa mfalme wa Uingereza kwenye safari kwenda Hispania. Mwaka uleule alifunga ndoa. Tangu 1367 alitajwa mara kwa mara kama mtumishi kwenye nyumba ya mfalme wa Uingereza akatumwa tena kama balozi kwenda nchi mbalimbali.

Tangu 1374 hadi 1385 alikuwa msimazi wa forodha kwenye bandari ya London. Baadaye akahamia mashambani aliposhika vyeo mbalimbali katika utumishi wa wafalme. Baada ya kifo chake alizikwa katika kanisa la Westminster Abbey.

Umuhimu wakle kwa fasihi ya Uingereza ni ya kwamba alikuwa kati ya waandishi wa kwanza waliotumia lugha ya Kiingereza. Hadi wakati wake lugha ya wasomi ilkuwa Kilatini au Kifaransa. Chaucer alitumia lugha ya watu wa kawaida (Kiingereza cha Kati) akainyosha kwa fasihi bora.

Pamoja na mashairi mbalimbali alitunga hasa masimulizi ya Canterbury Tales. Akiweka kwanza msingi wa kundi la wahiji wanaoelekea pamoja kusali kwenye kaburi la mtakatifu huko Canterbury kila mmoja kati ya hao anapewa kaziy a kusimulia hadithi. Kwa njia hii Chaucer aliunganisha hadithi nyingi juu ya msingi wa simulizi la safari ya pamoja. Hadithi hizi zimeonyesha pande zote za jamii ya Uingereza wa karne yake yaani maisha ya makabaila, wakulima, maskini na matajiri.

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Geoffrey Chaucer kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.