Hafni
Hafni (hafnium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Hafni (hafnium) |
Alama | Hf |
Namba atomia | 72 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 178.49 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 10, 2 |
Densiti | 13.31 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | {ugumu} |
Kiwango cha kuyeyuka | 2506 K (2233 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 4876 K (4603 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 4.9 * 1-4 % |
Hali maada | mango |
Hafni ni elementi na metali ya mpito yenye namba atomia 72 katika mfumo radidia. Jina latokana na "Hafnia" jina la Kilatini la mji wa Kopenhagen ilipogunduliwa mara ya kwanza.
Kutokea
Hafni hutokea ndani ya mitapo ya zirkoni tu. Uzalishaji wote duniani hauzidi tani 100 kwa mwaka. Hivyo bei yake ni juu.
Haitokeo katika mwili wa kibinadamu na hakuna habari ya kwamba ni sumu ndani yake.
Tabia
Rangi ni nyeupe-kijivu ikisafishwa. Haimenyuki kirahisi haivyo inatafutwa kwa aloi ambako kiasi kidogo chake huongeza uimara.
Hafni ina pia uwezo mkubwa wa kufyonza neutroni hivyo hutumiwa kwa nondo za kuendesha tanuri nyuklia.
Ikiwaka inatoa mwanga kali hivyo kuna matumizi katika mmweko wa picha.
-
Hafni tupu kando la sarafu
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hafni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |