Metali ya mpito

Kampaundi za metali za mpito zaonyesha rangi nyingi;
miyeyusho ya kamapaundi zifuatazo: [[Co(NO3)2]] (nyekundu); [[K2Cr2O7]] (machungwa); [[K2CrO4]] (njano); [[NiCl2]] (kijani); [[CuSO4]] (buluu); [[KMnO4]] (dhambarau).

Metali za mpito ni kundi la metali inayopatikana katikati ya jedwali la mfumo radidia wa elementi za kikemia. Zina tabia za kufanana. Ni elementi namba 21 hadi 30, 39 hadi 48, 57 hadi 80 na 89 hadi 112.

Zaitwa pia elementi za mpito lakini kwa sababu zote ni metali jina hili la "metali za mpito" ni kawaida vilevile. Jina latokana na tabia ya mzingo elektroni namba d katika atomi zao kutojaa nafasi zote za elektroni. Ndani ya kundi idadi ya elektroni katika nafasi ile huongezeka mfululizo kuanzia Skandi hadi Ununbi. Kwa hiyo kundi hili laonyesha mpito kutoka kundi la pili (Metali za udongo alikalini) hadi kundi la 13 (kundi la Boroni).

Kikemia metali ya mpito ni elementi yenye angalau ioni moja ya mzingo elektroni "d" usiojaa elektroni kwenye nafasi zote.

Kampaundi za metali za mpito mara nyingi huwa na rangi nyingi. Kwa mfano kampaundi za chuma huwa na rangi nyekundu au kijani; zile za kupri huwa ni nyeupe au kijani.

Isipokuwa Hidragiri zote ni katika hali mango kwa halijoto ya wastani.

Kundi 3 (III B) 4 (IV B) 5 (V B) 6 (VI B) 7 (VII B) 8 (VIII B) 9 (VIII B) 10 (VIII B) 11 (I B) 12 (II B)
Elementi ya radidi 4 Sc 21 Ti 22 V 23 Cr 24 Mn 25 Fe 26 Co 27 Ni 28 Cu 29 Zn 30
elementi radidi 5 Y 39 Zr 40 Nb 41 Mo 42 Tc 43 Ru 44 Rh 45 Pd 46 Ag 47 Cd 48
Elementi ya radidi 6 Lu 71 Hf 72 Ta 73 W 74 Re 75 Os 76 Ir 77 Pt 78 Au 79 Hg 80
Elementi ya radidi 7 Lr 103 Rf 104 Db 105 Sg 106 Bh 107 Hs 108 Mt 109 Ds 110 Rg 111 Uub 112
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Metali ya mpito kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.