Mama_wa_Mungu
Mwaka wa liturujia |
---|
Magharibi |
Mashariki |
Mama wa Mungu (kwa Kigiriki Θεοτόκος, Theotókos; kwa Kilatini Deipara au Dei genetrix, yaani "Mzaa Mungu") ni sifa kuu ambayo Wakristo wengi wanampatia Bikira Maria mama wa Yesu Kristo.
Msingi wa imani hiyo
Kwa kuwa wafuasi wa Yesu wanasadiki kuwa yeye ni Mungu sawa na Baba, wengi wao wanakubali kuwa aliyemzaa kama binadamu anastahili kuitwa Mama wa Mungu.
Dogma
Sifa hiyo ilianza kutumika katika karne ya 2, labda nchini Misri, ikathibitishwa moja kwa moja na Mtaguso wa Efeso (431) dhidi ya Patriarki Nestori aliyedai anaweza kuitwa tu Mama wa Yesu au Mama wa Kristo.
Mtaguso mkuu huo uliona kwamba Nestori alimgawa Yesu katika nafsi mbili: ya Kimungu na ya kibinadamu. Kumbe imani sahihi inamkiri kwamba nafsi ya Yesu ni ile ya Kimungu tu ambayo ni ya pili katika Utatu Mtakatifu. Hivyo aliyemzaa Yesu kama binadamu (si kama Mungu, jambo ambalo haliwezekani) anastahili kuitwa Mama wa Mungu (upande wa ubinadamu wake alioutwaa kwake).
Heshima katika sala
Kwa namna ya pekee, Maria anapewa sifa hiyo katika sala ya Salamu Maria, iliyo maarufu zaidi kati ya sala za Ukristo wa magharibi kwa mama wa Yesu.
Adhimisho katika liturujia
Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki wanaofuata mapokeo ya Kanisa la Roma tarehe 1 Januari, siku ya nane (Oktava) ya Noeli, lakini Wakatoliki wengine wanaiadhimisha siku tofauti, kwa mfano huko Milano ni Jumapili kabla ya Noeli.
Picha
-
Theotokos wa Vladimir
-
Theotokos wa Mt. Theodori
-
Theotokos Iverskaya, picha takatifu ya Kirusi ya karne ya 11, iliyotegemea nyingine ya karne ya 10, aina ya Hodegetria, Monasteri ya Iviron, Mlima Athos, Ugiriki.
-
Theotokos Panachranta alivyochorwa na Alipi wa Kiev
-
Blachernitissa
Marejeo
- Sirili wa Aleksandria, On the Unity of Christ, John Anthony McGuckin, trans. ISBN 0-88141-133-7
- McGuckin, John Anthony, St. Cyril of Alexandria: The Christological Controversy (1994, and reprinted 2004) ISBN 0-88141-259-7 A full description of the events of Third Ecumenical Council and the people and issues involved.
- John wa Shanghai na San Francisco,""The Orthodox Veneration of Mary, The Birth Giver of God"(2004, Sixth Printing, Third Edition). ISBN 0-938635-68-9
- Ware, Bishop Kallistos, "The Orthodox Way" (1979, Revised Edition, 1995, and reprinted 1999). ISBN 0-913836-58-3
- Maunder, Chris (ed.), The Origins of the Cult of the Virgin Mary , (2008, burns & oates/continuumbooks). ISBN 978-0-86012-456-6
Viungo vya nje
- Theotokos article on the Orthodox Wiki
- Resources on the Theotokos Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Study of the Mother of the Lord the All-Holly Theotokos and Ever-Virgin Mary Ilihifadhiwa 19 Julai 2006 kwenye Wayback Machine. by St. Nectarios (in Greek)
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mama wa Mungu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |