Maria wa Bethania
Maria wa Bethania (jina lake kwa Kiebrania מִרְיָם, Miryām, kwa Kiaramu מרים, Maryām, kwa Kigiriki Μαρία, Maria) alikuwa mwanamke wa Bethania, kitongoji cha Yerusalemu, katika karne ya 1[1].
Ndugu zake walikuwa Martha na Lazaro wa Bethania, ambao wote Yesu alifurahia urafiki wao hasa alipohiji kwenda Yerusalemu.
Wanaheshimiwa na Wakristo wengi kama watakatifu[2].
Sikukuu yao inaadhimishwa pamoja tarehe 29 Julai[3] au 4 Juni, kadiri ya madhehebu.
Maisha
Anajulikana hasa kutokana na Injili, kwa namna ya pekee Injili ya Luka (10:38-42) na Injili ya Yohane (11; 12:1-8), katika Agano Jipya ndani ya Biblia ya Kikristo.
Humo anaonekana mwenye silika ya utulivu na imani kwa Yesu Kristo, ambaye alipendezwa sana na usikivu wake wakati alimfundisha ameketi chini karibu na miguu yake, kama ilivyokuwa kawaida ya wanafunzi wa dini ya Kiyahudi, ingawa wakati huo wanaume tu walikubalika.
Tazama pia
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
Viungo vya nje
- Easton's Bible Dictionary, 1897
- Catholic Encyclopedia 1910: under "Saint Mary Magdalene"
- Mary & Martha, the sisters of Lazarus Archived 26 Oktoba 2009 at the Wayback Machine., Greek Orthodox Archdiocese of America.
- CIRCULO SANTA MARIA DE BETANIA, group dedicated to the devotion of Saint Mary of Bethany in the Philippines
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maria wa Bethania kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |