Kaunti ya Kisii
Kaunti ya Kisii ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,266,860 katika eneo la km2 1,323, msongamano ukiwa hivyo wa watu 958 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Kisii.
Utawala
Kaunti ya Kisii ina maeneo bunge yafuatayo[2]:
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]
- Etago 83,787
- Gucha 83,740
- Gucha South 83,623
- Kenyenya 131,740
- Kisii Central 166,906
- Kisii South 135,134
- Kitutu Central 154,175
- Marani 107,464
- Masaba South 122,396
- Nyamache 130,898
- Sameta 66,99
Uchumi
Wakazi wengi wa kaunti hii wanategemea kilimo kwa chakula na mapato ya kifedha. Baadhi ya mimea inayokuzwa ni mahindi, ndizi na chai.[4].
Pia kuna biashara, hasa uuzaji wa mazao ya kilimo.
Tazama pia
- Mji wa Kisii
- Orodha ya mito ya kaunti ya Kisii
- Wilaya ya Gucha (Kisii Kusini)
- Wilaya ya Nyamira (Kisii Kaskazini)
- Wilaya ya Kisii Kati
Marejeo
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ http://countytrak.infotrakresearch.com/Kisii-county/
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ Ripoti ya Ufugaji wilayani Kisii: www.smallholderdairy.org
Viungo vya Nje
- Tovuti ya Kisii.com
- NPR Masimulizi kuhusu Lugha ya Kikisii
- Mradi wa Fulda-Mosocho Archived 22 Julai 2015 at the Wayback Machine.